Vijana
wa Kundi la 4U Movement, liliokuwa likimuunga mkono Waziri Mkuu wa
zamani Edward Lowassa, washangilia baada kuzungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana kuhusu msimamo wao wa kuungamkono UKAWA.
4U Movement | FRIENDS OF LOWASSA
Utumishi, Uwajibikaji, Uzalendo na Umoja
Saturday, 18 July 2015
Thursday, 9 July 2015
Shukrani za Mh. Rais Kikwete kwa Mh. Edward Ngoyai Lowassa
Mh. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe
(9/7/2015) akiwa ndani ya bunge kwa ajili ya kulivunja bunge, pamoja na kutaja
changamoto nyingi na mafanikio ya serikali ya awamu ya nne, Mh Jakaya Mrisho
Kikwete alisema maneno yafuatayo
"Natambua kazi kubwa aliyoifanya Edward Lowassa kwa
kipindi kifupi alipokuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,
Namshukuru saana"
Haya ni maneno mazito saana na yenye dhamani saana kutoka kwa rais wa nchi yetu akitambua mchango wa rafiki yetu na mpendwa wetu Mh. Edward Lowassa, hivyo basi mchango na uchapakazi wa Edward Lowassa unajulikana na unatambulika saana na kueshimiwa pia. 4U Movement tunaye mtu wa kuipeleka nchi kwenye maendeleo ya kasi zaidi, maendeleo tunayoyahitaji, ambayo yatajengwa kwenye msingi wa sasa.
Wednesday, 8 July 2015
TAARIFA KWA 4U MOVEMENT
Habari,
Wana 4U Movement mliopo Dodoma na watanzania wote wenye mapenzi mema na Mh. Edward
Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4U Movement au zenye jina la Edward
Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoendelea hapa Dodoma. Najua na kutambua hadi jana
tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4U Movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini
wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya aina yeyote.
Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4U Movement kufanya vurugu ndani ya mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea heshima, sifa ya utulivu na umakini 4U Movement. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa mbele kumshughulikia. Tunawaasa na kuwaomba wana 4U Movement na watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi wajumbe wote wa vikao vya maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa utulivu.
Maana ule wakati wa mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa muda ukifika basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukiyakosa tutayapata nje ya CCM, lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM chini ya balozi wetu wa 4U Movement Mh Edward Lowassa.

Ahsanteni
Hemedy
AllyMratibu Taifa (National Coordinator)
@4u
movement
# UTUMISHI# UWAJIBIKAJI# UMOJA# UZALENDO
# UTUMISHI# UWAJIBIKAJI# UMOJA# UZALENDO
Monday, 6 July 2015
TAARIFA MUHIMU KWA 4U MOVEMENT TANZANIA
Habari Tanzania, ni miaka mitatu tangu kuanza kwa 4U movement Tanzaniatukipigania kwa jasho na damu, kudai haki na uhuru wa kweli chini ya balozi wa UTUMISHI, UWAJIBIKAJI, UMOJA NA UZALENDO wa kweli Mh. Edward Ngoyai Lowassa. Kazi ambayo tuliifanya na tunaendelea kuifanya kwa moyo na uzalendo kwa Taifa letu.
Monday, 15 June 2015
Mh.Lowassa akutana na mafuriko ya Bukoba
Mh.Lowassa leo amekutana na wananchi wa Bukoba, wananchi wametokseza wengi saana kwa ajili ya kuongea na Mh. Lowassa na kumdhamini, Tunawashukuru saana wananchi wa Kagera kwa kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha safari yetu ya Matumaini
Wananchi wa Bukoba wakisalimiana na mh. Lowassa baada ya kufika Bukoba akitokea Kigoma |
Saturday, 13 June 2015
Daaah, Kigoma nako wametisha
Mh. Lowassa leo alikuwa kigoma kutafuta wadhamini, kwakweli hali ilivyokuwa ni ajabu saana. watu ni wengi saana tena saana wakitaka kuongea na Mh.Lowassa kila mahali, tunawashukuru saana wana Kigoma kwa kuungana na Mh.Lowassa katika safari hii ya matumaini
Umati wa watu ni mkubwa sana uliojitokeza kwenye ofisi za CCM mkoa kumdhamini mh. Lowassa |
Friday, 12 June 2015
Mafuriko ya Tabora yafunika
mh. Lowassa ameendelea kuonyesha kuwa yeye ndo tegemeo na kiongozi anayehitajika kwa sasa Tanzania, hii imetokea mkoani Tabora baada ya watu wengi saana kujitokeza kutaka kumuona na kuzungumza naye. Pamoja na kuhitaji wadhamini 30 tu kila mkoa. Mh Lowassa jana amevunja record yake mwenyewe ya kupata wadhamini wengi baada ya kupata wadhamini zaidi ya 9000 mkoani Tabora, hii kweli inaonyesha watanzania wanamuhitaji kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania
Mkoani Tabora, wananchi wamejitokeza kwa wingi saana kumdhamini mh. Lowassa na kuonyesha kuwa Lowassa ndo kipenzi chao |