Wednesday, 8 July 2015

TAARIFA KWA 4U MOVEMENT

Habari, Wana 4U Movement mliopo Dodoma na watanzania wote wenye mapenzi mema na Mh. Edward Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4U Movement au zenye jina la Edward Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoendelea hapa Dodoma. Najua na kutambua hadi jana tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4U Movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya aina yeyote. 

Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4U Movement kufanya vurugu ndani ya mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea heshima, sifa ya utulivu na umakini 4U Movement. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa mbele kumshughulikia. Tunawaasa na kuwaomba wana 4U Movement na watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi wajumbe wote wa vikao vya maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa utulivu. 

Maana ule wakati wa mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa muda ukifika basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukiyakosa tutayapata nje ya CCM,  lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM chini ya balozi wetu wa 4U Movement Mh Edward Lowassa.

Ahsanteni 
Hemedy AllyMratibu Taifa (National Coordinator)

@4u movement
# UTUMISHI# UWAJIBIKAJI# UMOJA# UZALENDO

No comments:

Post a Comment

4U Movement wanakuomba kufuata maadili ya Kitanzania, Karibu !