Monday, 6 July 2015

TAARIFA MUHIMU KWA 4U MOVEMENT TANZANIA

Habari Tanzania, ni miaka mitatu tangu kuanza kwa 4U movement Tanzaniatukipigania kwa jasho na damu, kudai haki na uhuru wa kweli chini ya balozi wa UTUMISHI, UWAJIBIKAJI, UMOJA NA UZALENDO wa kweli Mh. Edward Ngoyai Lowassa. Kazi ambayo tuliifanya na tunaendelea kuifanya kwa moyo na uzalendo kwa Taifa letu.
Misingi yetu haifungamani na chama chochote cha siasa na falsafa hii imemjengea mh. Edward Lowassa wafuasia na marafiki wengi nje na ndani ya chama chake.

Kwa umuhimu wa kutambua kuwa vikao vya chama cha mapinduzi (CCM) ambavyo vitapelekea kutangazwa kwa mgombea atakae peperushabendera ya chama cha mapinduzi, tunaombwa tufanye yafuatayo kwa misingi yetu ya kujitolea.


  1. Tunawaomba na kuwahamasisha watanzania wenye kuitakia Tanzania mema kuungana na wana 4U movement million 5 kujumuika na wanachama wa chama cha mapinduzi kuja Dodoma kwa gharama za kujitolea wenyewe kama kawaida yetu ili kuungan ana 4U movement 2000 waliotangulia kuwasili bila kubughudhi au kuvunja sheria za Nchi.
  2. Tunawaomba wana 4U movement kuendelea kusali na kuomba dua kwa Mwenyezi  Mungu ailinde Amani ya Nchi yetu Tanzania na kuivusha salama  safari ya Matumaini ya rafiki yetu, mpendwa wetu, kiongozi wetu mh. Edward Ngoyai Lowassa
  3. Kuwa makini saana  na kutokuwa na hofu kwa aina zozote za propaganda zinazoendelea katika mitandao ya kijamii kwani vikao halali vya chama  cha mapinduzi havijakaa kujadili hatma ya wagombea wote nani wa kuibeba bendera ya CCM, tuwe watulivu tukisubilia kutangazwa rasmi kwa mh. Edward Ngoyai Lowassa kuwa mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi.


Mwisho
Tunamtakia  afya njema Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wajumbe woote wa vikao vya maamuzi katika kipindi hiki ambacho kitatupa hatma ya Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo.

Karibu wana 4U movement Dodoma, kushuhudia matunda ya kazi ya mikono damu na jasho letu.

Ahsanteni

Mr Hemed Ally
Mratibu Taifa (Nation Coordinator)
@4U Movement

#UTUMISHI         #UWAJIBIKAJ     I #UMOJA     #UZALENDO

No comments:

Post a Comment

4U Movement wanakuomba kufuata maadili ya Kitanzania, Karibu !