Saturday 18 July 2015

KUNDI LA VIJANA LA 4U MOVEMENT LATANGAZA KUUNGA MKONO UKAWA, AWALI LILIKUWA LIKIMUUNGA MKONO LOWASSA

Vijana wa Kundi  la 4U Movement, liliokuwa likimuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, washangilia baada kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu msimamo wao wa kuungamkono UKAWA.

Thursday 9 July 2015

Shukrani za Mh. Rais Kikwete kwa Mh. Edward Ngoyai Lowassa

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe (9/7/2015) akiwa ndani ya bunge kwa ajili ya kulivunja bunge, pamoja na kutaja changamoto nyingi na mafanikio ya serikali ya awamu ya nne, Mh Jakaya Mrisho Kikwete alisema maneno yafuatayo

"Natambua kazi kubwa aliyoifanya Edward Lowassa kwa kipindi kifupi alipokuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Namshukuru saana"


Haya ni maneno mazito saana na yenye dhamani saana kutoka kwa rais wa nchi yetu akitambua mchango wa rafiki yetu na mpendwa wetu Mh. Edward Lowassa, hivyo basi mchango na uchapakazi wa Edward Lowassa unajulikana na unatambulika saana na kueshimiwa pia. 4U Movement tunaye mtu wa kuipeleka nchi kwenye maendeleo ya kasi zaidi, maendeleo tunayoyahitaji, ambayo yatajengwa kwenye msingi wa sasa.

Wednesday 8 July 2015

TAARIFA KWA 4U MOVEMENT

Habari, Wana 4U Movement mliopo Dodoma na watanzania wote wenye mapenzi mema na Mh. Edward Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4U Movement au zenye jina la Edward Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoendelea hapa Dodoma. Najua na kutambua hadi jana tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4U Movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya aina yeyote. 

Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4U Movement kufanya vurugu ndani ya mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea heshima, sifa ya utulivu na umakini 4U Movement. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa mbele kumshughulikia. Tunawaasa na kuwaomba wana 4U Movement na watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi wajumbe wote wa vikao vya maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa utulivu. 

Maana ule wakati wa mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa muda ukifika basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukiyakosa tutayapata nje ya CCM,  lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM chini ya balozi wetu wa 4U Movement Mh Edward Lowassa.

Ahsanteni 
Hemedy AllyMratibu Taifa (National Coordinator)

@4u movement
# UTUMISHI# UWAJIBIKAJI# UMOJA# UZALENDO

Monday 6 July 2015

TAARIFA MUHIMU KWA 4U MOVEMENT TANZANIA

Habari Tanzania, ni miaka mitatu tangu kuanza kwa 4U movement Tanzaniatukipigania kwa jasho na damu, kudai haki na uhuru wa kweli chini ya balozi wa UTUMISHI, UWAJIBIKAJI, UMOJA NA UZALENDO wa kweli Mh. Edward Ngoyai Lowassa. Kazi ambayo tuliifanya na tunaendelea kuifanya kwa moyo na uzalendo kwa Taifa letu.

Monday 15 June 2015

Mh.Lowassa akutana na mafuriko ya Bukoba

Mh.Lowassa leo amekutana na wananchi wa Bukoba, wananchi wametokseza wengi saana kwa ajili ya kuongea na Mh. Lowassa na kumdhamini, Tunawashukuru saana wananchi wa Kagera kwa kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha safari yetu ya Matumaini

Wananchi wa Bukoba wakisalimiana na mh. Lowassa baada ya kufika Bukoba akitokea Kigoma

Saturday 13 June 2015

Daaah, Kigoma nako wametisha

Mh. Lowassa leo alikuwa kigoma kutafuta wadhamini, kwakweli hali ilivyokuwa ni ajabu saana. watu ni wengi saana tena saana wakitaka kuongea na Mh.Lowassa kila mahali, tunawashukuru saana wana Kigoma kwa kuungana na Mh.Lowassa katika safari hii ya matumaini
Umati wa watu ni mkubwa sana uliojitokeza kwenye ofisi za CCM mkoa kumdhamini mh. Lowassa

Friday 12 June 2015

Mafuriko ya Tabora yafunika

mh. Lowassa ameendelea kuonyesha kuwa yeye ndo tegemeo na kiongozi anayehitajika kwa sasa Tanzania, hii imetokea mkoani Tabora baada ya watu wengi saana kujitokeza kutaka kumuona na kuzungumza naye. Pamoja na kuhitaji wadhamini 30 tu kila mkoa. Mh Lowassa jana amevunja record yake mwenyewe ya kupata wadhamini wengi baada ya kupata wadhamini zaidi ya 9000 mkoani Tabora, hii kweli inaonyesha watanzania wanamuhitaji kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania

Mkoani Tabora, wananchi wamejitokeza kwa wingi saana kumdhamini mh. Lowassa na kuonyesha kuwa Lowassa ndo kipenzi chao

Mafuriko ya Nzega yatisha

Watu wengi saana wamejitokeza leo katika zoezi la kumdhamini mh. Lowassa huko Nzega, hali hii ni ya kutia matumaini sana, kweli Nguvu ya Umma imeamua kuleta mabadiriko kupitia kwa mh.Lowassa


Vijana wa Nzega wamkalibisha mh.Lowassa kwa ujumbe wa kumuomba aendelee kuwapigania

Wilaya ya Nzega wamsubilia Mh. Lowassa Barabarani

Wananchi wa kijiji cha Nata, wilaya ya Nzega wamsubilia mh.Lowassa barabarani ili waweze kumuona na kumsalimia

Mh. Lowassa akiwasalimia wananchi wa Nata


Wednesday 10 June 2015

4U Movement wakiwa mkoani Simiyu

4U movement jumatano tarehe 10 2015 waliungama mh. Lowassa moani Simiyu kuhakikisha kazi ya kuwapata wadhamini inakuwa rahisi kabisa. vijana hao kwa nia moja ya kuliletea maendeleo Taifa la Tanzania wameendelea kuifanya kazi bila kuchoka
4U Movement wakiwa ndani ya Simiyu tayari kabisa kumpokea mh. Lowassa
Thanks Saana 4U Movement Simiyu kwa kazi nzuri.

MAFURIKO YA LOWASSA NDANI SIMIYU

Mh. Edward Lowassa, akiwa juu ya gari lake, akiwapungia mamia ya wana CCM waliofika kumdhamini huko Lamadi, wilaya ya Busega mkoani Simiyu, pamoja na wananchi wengine. Mh. Lowassa, aliwasili huko Jumatano Juni 10, 2015. Mh Lowassa kwa sasa anaendelea na zoezi la kutafuta wadhamini kanda ya ziwa

Mh. Lowassa akiwasalimia wananchi waliojitokeza kumlaki huko Simiyu

Simiyu tunawashukuru saana, mmetupokea vizuri na mmeonyesha kuwa mto na sisi katika safari ya matumaini ya mh. Lowassa.

Bariadi nako Wafunika

Wana bariadi nao hawakuwa nyuma katika kumpokea mpendwa wao Mh. Edward Ngoyai Lowassa Watu wamejitokeza kwa wingi kuhakikisha zile sahihi 450 zinapatikana kirahisi saana Tunawashukuru saana na tuko pamoja nanyi katika safari yetu hii ya matumaini kwa Watanzania
Hivi ndivyo ilivyokuwa huko Bariadi katika kumdhamini Mh. Lowassa

4U Movement watoa semina elekezi Same kuhusu umuhimu wa kupiga kura

4U Movement ndani ya Same leo, tukitoa semina kwa marafiki wa Lowassa juu ya umuhimu wa kujihandikisha kwenye daftari la kudumu, umuhimu wa kupiga kura na kujagua viongozi bora kwa ajili ya maendeleo ya Taifa, na baadae tulitembelea Gereza la Same na kutoa Misaada ya kijamii kwa wafungwa.
4U Movement wakitoa semina kuhusu upigaji wa kura

4U Movement wakitoa Misaada Gereza la Samae

Happy Birth Mama Regina Lowassa
































Best Wishes from Fans

We love you forever and ever. No matter where we go or whom we meet, you will always be Number One to us.

Tuesday 9 June 2015

Mh. Lowassa akiwa ndani ya Bunda

Baada ya kutoka Musoma, Mh. Lowassa alikwenda Bunda nako kuomba wapendwa kumdhamini katika safari ya matumaini
Nako kulikuwa hivi
Haya ndo mafuriko ya Bunda

Edward Lowassa Leo akiwa Musoma

Mh. Lowassa leo yuko Musoma akikutana na wananchi kwa ajili ya kuwaomba wamdhamini katika safari yake ya matumaini
Hali ilikuwa kama hivi
Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wananchi kabla

Wananchi wamepanga mstari wakimsubilia Mh. Edward Lowassa



4U Movement