Saturday 18 July 2015

KUNDI LA VIJANA LA 4U MOVEMENT LATANGAZA KUUNGA MKONO UKAWA, AWALI LILIKUWA LIKIMUUNGA MKONO LOWASSA

Vijana wa Kundi  la 4U Movement, liliokuwa likimuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, washangilia baada kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu msimamo wao wa kuungamkono UKAWA.

Thursday 9 July 2015

Shukrani za Mh. Rais Kikwete kwa Mh. Edward Ngoyai Lowassa

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe (9/7/2015) akiwa ndani ya bunge kwa ajili ya kulivunja bunge, pamoja na kutaja changamoto nyingi na mafanikio ya serikali ya awamu ya nne, Mh Jakaya Mrisho Kikwete alisema maneno yafuatayo

"Natambua kazi kubwa aliyoifanya Edward Lowassa kwa kipindi kifupi alipokuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Namshukuru saana"


Haya ni maneno mazito saana na yenye dhamani saana kutoka kwa rais wa nchi yetu akitambua mchango wa rafiki yetu na mpendwa wetu Mh. Edward Lowassa, hivyo basi mchango na uchapakazi wa Edward Lowassa unajulikana na unatambulika saana na kueshimiwa pia. 4U Movement tunaye mtu wa kuipeleka nchi kwenye maendeleo ya kasi zaidi, maendeleo tunayoyahitaji, ambayo yatajengwa kwenye msingi wa sasa.

Wednesday 8 July 2015

TAARIFA KWA 4U MOVEMENT

Habari, Wana 4U Movement mliopo Dodoma na watanzania wote wenye mapenzi mema na Mh. Edward Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4U Movement au zenye jina la Edward Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoendelea hapa Dodoma. Najua na kutambua hadi jana tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4U Movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya aina yeyote. 

Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4U Movement kufanya vurugu ndani ya mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea heshima, sifa ya utulivu na umakini 4U Movement. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa mbele kumshughulikia. Tunawaasa na kuwaomba wana 4U Movement na watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi wajumbe wote wa vikao vya maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa utulivu. 

Maana ule wakati wa mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa muda ukifika basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukiyakosa tutayapata nje ya CCM,  lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM chini ya balozi wetu wa 4U Movement Mh Edward Lowassa.

Ahsanteni 
Hemedy AllyMratibu Taifa (National Coordinator)

@4u movement
# UTUMISHI# UWAJIBIKAJI# UMOJA# UZALENDO

Monday 6 July 2015

TAARIFA MUHIMU KWA 4U MOVEMENT TANZANIA

Habari Tanzania, ni miaka mitatu tangu kuanza kwa 4U movement Tanzaniatukipigania kwa jasho na damu, kudai haki na uhuru wa kweli chini ya balozi wa UTUMISHI, UWAJIBIKAJI, UMOJA NA UZALENDO wa kweli Mh. Edward Ngoyai Lowassa. Kazi ambayo tuliifanya na tunaendelea kuifanya kwa moyo na uzalendo kwa Taifa letu.